come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KIIZA AIVUTIA PUMZI AZAM JUMAMOSI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Hamis Kiiza (Pichani), alianza mazoezi na wenzake kwenye Uwanja wa Loyola jana, tayari kwa maandalizi ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kupigwa Jumamosi hii Uwanja wa Taifa.


Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kaziguto, aliupasha mtandao huu kuwa Kiiza amejumuika na wenzake baada ya kuomba ruhusa katika timu yake ya taifa, Uganda, ‘The Cranes’.

Kaziguto alisema kikosi chao kwa sasa kimekamilika baada ya Kiiza kuwasili na wanaendelea na maandalizi na mchezo huo ambao ni muhimu kwao kama mabingwa msimu uliopita.

“Kiiza leo ameanza mazoezi na wenzake, tayari kwa mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Azam FC na sisi tumejiandaa na tunaendelea kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo na tunamshukuru Mungu hatuna majeruhi hata mmoja katika kikosi chetu,” alisema Kaziguto.

Wakati Yanga wakiendelea kujifua kwa ajili ya mchezo huo, nao Azam FC jana waliingia kambini Chamazi nje kidogo ya jiji mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika Kusini walikokuwa kwa ziara ya siku 12.

Meneja wa Azam FC, Jemedari Saidi, alisema maandalizi waliyoyafanya na mechi walizocheza zinawatosha na sasa wanaendelea na mazoezi hadi siku ya mchezo huo.