Nahodha msaidizi wa mabingwa wa soka nchini Yanga Haruna Niyonzima 'Fabregas', amewaahidi wapenzi na mashabiki wa Yanga ushidni mnono kwenye mechi nyingine ya mzunguko wa pili kati yao na Coastal Union ya Tanga utakaopigwa Jumatano ijayi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana mara baada ya kumalizika mchezo wao dhidi ya Ashanti ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 5-1, Niyonzima amesema kuwa kikosi chao cha Yanga kimeimaiika idara zote hivyo haoni sababu ya kutoibuka na ushindi.
'Yanga ina kikosi bora kwa sasa hilo halipingiki na ushindi ni wetu dhidi ya Coastal' alisema Niyonzima.