come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

HATIMAYE RIDHA WAENDA URUSI LEO



Wanariadha wawili wanaounda timu ya taifa ya mchezo huo wanatarajia kuondoka nchini leo kuelekea jijini Moscow, Urusi kushiriki michuano ya mbio za dunia inayoendelea kufanyika nchini humo, imeelezwa.


Wanariadha hao ambao wote watawania medali katika mbio ndefu ni Mohamed Msenduki na Faustine Mussa.

Akizungumza jana Katibu wa Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui (Pichani), alisema kuwa awali wanariadha hao walitakiwa kuondoka nchini tangu Agosti 7, lakini safari yao ikaahirishwa na sasa watasafiri leo huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri wakati watakapokimbia Agosti 17.

"Vijana hawa ni wazuri na tunaamini kuwa watatuwakilisha vyema," alisema Nyambui.

RIADHA PWANI
Timu ya riadha ya mkoa wa Pwani imewataka wadau wa mkoa huo wajitokeze kuwasaidia fedha kwa ajili ya maandalizi ya mashindno ya riadha ya taifa yaliyopangwa kufanyika Agosti 23 na 24 kwenye Uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro. Kikosi cha timu hiyo kinatarajia kwenda Morogoro kikiwa na wanariadha 20.

Kocha wa timu ya riadha ya Pwani, Robert Kalyahe, alisema kuwa hadi sasa timu yao inaendelea na mazoezi ingawa bado haijapata fedha kwa ajili ya maandalizi na ushiriki wa mashindano hayo ya taifa, hivyo akawataka wadau wa michezo mkoani Pwani kujitokeza ili kuwaunga mkono.