Mechi ya mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Rhino Rangers dhidi ya Simba iliyomalizika kwa sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi imeweka rekodi ya kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kwenye uwanja huo uliojengwa 1987.
Akizungumza mjini Tabora jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora (Tarefa), Fateh Remtura, alisema mechi hiyo ya ligi kuu iliyokuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo tangu timu ya Milambo ishuke daraja miaka 14 iliyopita imeingiza Sh. milioni 44.8.
Remtura alisema mechi hiyo ilishuhudiwa na watazamaji 12,981 waliokata tiketi za Sh. 3,000 na 5,000 huku kila timu ikipata Sh. 10,002,925.
“Rekodi zilizopo zinaonyesha kiingilio cha juu kilichowahi kukusanywa kwenye uwanja wetu (Ali Hassan Mwinyi) ni Sh. milioni 17,” alisema Remtura.
Tarefa wamepataa mgawo wa Sh. 1,186,787 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani imekatwa Sh. 8,680,878.
Mgawo mwingine wa mechi hiyo ni uwanja Sh. 5,086233, gharama za mechi Sh. 3,510,739, Kamati ya Ligi Sh. 3,510,739, gharama za tiketi Sh. 2,540,000, mtathimini wa marefa Sh. 310,000 na Mfuko wa Maendeleo ya Soka (FDF) Sh. 1,525,869.
YANGA MIL. 102
Mechi nyingine ya Ligi Kuu kati ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Ashanti United iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza Sh. milioni 102.8. Katika mechi hiyo, Yanga iliibuka na ushindi wa magoli 5-1.
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa mechi iliingiza kiasi hicho cha fedha kutokana na mashabiki 17,744 waliokata tiketi kuishuhudia.
Alisema kuwa viingilio katika mechi hiyo vilikuwa Sh. 5,000, Sh. 8,000, Sh. 15,000 na Sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa Sh. 24,400,102.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni Sh. 15,689,898.31.
Alisema kuwa mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja Sh. 12,406,831.75, tiketi Sh. 4,453,890, gharama za mechi Sh. 7,444,099.05, Kamati ya Ligi Sh. 7,444,099.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh. 3,722,049.53 na Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh. 2,894,927.41.
“Tulistahili kushinda lakini kipa wetu (Dhaira) hakucheza vizuri. Hakuwa sawa sawa. Tuna makipa watatu, mechi ijayo tutaangalia namna ya kufanya,” alisema Kibadeni.
Aidha, kocha aliyejiunga na Simba baada ya kumalizika kwa msimu uliopita wa ligi hiyo akitokea Kagera Sugar, alisema maamuzi ya kuwazuia kucheza nyota wao Warundi Gilbert Kaze na Amisi Tambwe yaliyochukuliwa na TFF jana mchana, yalichangia kuzorotesha kikosi chake.
“Tulikuwa tumewaandaa wale vijana (Kaze na Tambwe) kwa ajili ya mechi lakini saa saba mchana tukaambiwa ITC zao hazijafika na haturuhusiwi kuwachezesha.
Imetuharibia mipango ya timu yetu,” alisema Kibadeni katika kauli ambayo ilionyesha kukosa mawasiliano na uongozi wake hasa kamati ya usajili ya Simba.
Simba iliondoka mjini hapa jana asubuhi kwenda jijini Arusha tayari kwa mechi yao ya pili ya ligi hiyo dhidi ya Oljoro JKT, ambayo juzi ilianza vibaya baada ya kukubali kichapo cha 2-0 nyumbani dhidi Coastal Union.
Rhino, ambao wameweka kambi yao maeneo ya Ipuli takriban Km 6 kutoka Tabora Mjini, jana asubuhi waliendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini hapa kujiandaa kwa mechi yao ya pili dhidi ya Azam, ambao juzi walianza kwa sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa wa 1999 na 2000 wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar.