Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga (Pichani), leo wanashuka dimbani kuwania Ngao ya Jamii kwenye uwanja wa Taifa dhidi ya Azam FC majira ya saa 10:30 Arasili ambapo imeahidi ushindi mnono na kuwapa raha mashabiki wake.
Akizungumza mapema leo asubuhi, Msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto 'Kizu' amedai kuwa Yanga inaweza kushinda mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri iliyofanya msimu huu.
Ameongeza kuwa kikosi cha Azam hakijabadilika hivyo ni moja kati ya sababu ya kuwafunga, anaongeza kuwa msimu uliomalizika Yanga iliweza kuifunga Azam mara zote mbili na kutwaa ubingwa wa Tanzania bara hivyo haoni sababu ya kuukosa ushidni jioni ya leo.
Aidha msemaji huyo amedai kukosekana kwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa hakutawaangusha katika mchezo huo kwani waliweza kuifunga Azam bila ya kuwepo Ngassa, 'Yanga ni timu bora kwa sasa hapa nchini lakini licha ya ubora tunaiheshimu sana Azam ila lazima tuwafunge', alisisitiza Kizuguto.
Yanga leo itashuka dimbani bila ya straika wake Mrisho Ngassa ambaye amefungiwa mechi sita kwa kosa la kusaini timu mbili, lakini itawatumia washambuliaji wake mahiri Didier Kavumbagu, Jerry Tegete, Hamis Kiiza na Hussein Javu