Kocha msaidizi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga, Fred Felix Minziro (Pichani) ameonyesha masikitiko yake juu ya mwamuzi wa mchezo wa jana wa ligi kuu kati yao na Coastal Union ya Tanga uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa ambapo aliwapa penalti ya utata na kuwalazimisha sare ya 1-1.
Minziro amedai Coastal Union ilibebwa na mwamuzi wa mchezo huo Martin Saanya, 'Mwamuzi wa mchezo hakutenda haki amewapa penalti Coastal, mpira ulimgonga Haruna Niyonzima mgongoni nashangaa akapuliza kipyenga kuashilia penalti wakati yeye akuwepo eneo la tukio', alisema Minziro.
Kocha huyo msaidizi wa Yanga mwenye hasira ameendelea kulia na waamuzi wa soka ambao wanavunja sheria za mchezo huo na kukandamiza maendeleo ya soka hapa nchini, Anaongeza kuwa Coastal Union ilipaswa kutafuta goli kwa juhudi zao binafsi ama kupata penalti isiyo na utata, Lakini kitendo alichofanya mwamuzi huyo kinaashilia kukandamiza soka nchini.
Minziro amelitaka shirikisho la kandanda nchini TFF kupanga waamuzi wenye weledi na kazi yao na si kukurupuka kuwaletea waamuzi wanaochezesha kiushabiki pasipo kufuata sheria za FIFA