Balotelli, ambaye amefunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, alishuhudia mkwaju wake ukiokolewa na kipa Pepe Reina dakika ya 60.
Hata hivyo, 'Supermario' aliifungia Milan dakika ya 90 na ushei kabla ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje mwishoni mwa mchezo. Mabao ya Napoli yalifungwa na Britos dakika ya sita na HiguaĆn dakika ya 54 pasi ya Zuniga.