Mara baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-2 toka kwa Azam Fc wazee wa klabu ya Yanga wamesema hakuna mchawi ndani ya timu hiyo isipokuwa ni sehemu ya mchezo tu, wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu wamedai kwa sasa Yanga hakuna mchawi na ieleweke hivyo.
Wameongeza wanashangaa kila matokeo yanapoelekea mabaya kwa upande weao huanza kuwatazama kwa jicho lingine, wamesema Yanga kutoka sare tatu mfululizo na kufungwa na sehemu ya mchezo kwani ndio yalivyo matokeo.
'Siku zote katika mchezo wa soka kuna matokeo aina tatu kufungwa, sare na kushinda, lakini tunashangaa kwamba kufanya vibaya kwa Yanga lawama zote tunapelekewa sisi, sisi hatujavua kofia na ombi letu la kuwataka viongozi wasimpe ajira Mkenya limetekelezwa kwani hujui kama Mkenya si katibu?, alihoji mzee mmoja aliyekataa kutaja jina lake.
Aidha wazee wengine wa Yanga wamewataka wachezaji wa timu hiyo kujituma ili kuweza kuibuka na ushindi na wasitegemee imani nyingine, ameendelea kudai mpira wa siku hizi unachezwa kisayansi na masuala ya kutegemea nguvu za giza yamepitwa na wakati