Kauli hiyo ya Kibadeni imekuja mara baada ya kuona wachezaji wakionesha viwango tofauti kila kukicha kwamba leo wanaweza kucheza vizuri na kesho wakacheza hovyo, akisema kwa timu inayopigania mafanikio ya kweli, hilo si zuri kwani timu inatakiwa iwe na uwezo kamili.
Kibadeni alisema anashindwa kujua tatizo la vijana wake kwani hakuvutiwa na kiwango cha timu yake katika mechi ya juzi dhidi ya Mafunzo japo walishinda kwani hakuna kilichoongezeka kiuchezaji ni kama walivyocheza na JKT Oljoro waliposhinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, Agosti 28.
Alisema, kwa sasa ana kazi kubwa ya kufanya maboresho kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Septemba 14 katika dimba la Taifa, Dar es Salaam ili makosa aliyoyaona juzi yasije yakajirudia.