come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MZEE KINESI AWACHAFUA LIPULI

Uongozi wa klabu ya Simba umeingia matatani kufuatia viongozi wa timu ya Lipuli ya Iringa kudai kuibiwa fedha zao za mgao takribani shilingi milioni mbili wakati wa mechi yao ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Kinesi.


Katika mchezoi huo wa kujipima nguvu ambapo Simba ilishinda magoli 2-0, inadaiwa makamu mwenyekiti wa Simba Joseph Itang'are maarufu mzee Kinesi kuwaingiza mitini mapato ya mchezo huo na kujikuta wakiambulia laki sita tu badala ya milioni mbili.

Hata hivyo Mzee Kinesi alikanusha malalamiko yanayotolewa na viongozi wa Lipuli na kudai yeye hakuhusika katika kusimamia viingilio, lakini Lipuli wanadai kwamba mzee Kinesi na viongozi wengine walikutumika kuwahujumu katika mapato.

Wanadai kwamba viongozi hao wa Simba kila mmoja alikuwa na daftari la kwake linaloashilia mapato ya mechi hiyo huku pia familia ya mzee huyo nayo ikihusika