Msimamo huo umeendelea kusisitizwa na baadhi ya wajumbe kwenye baraza hilo la wazee ambalo limejipatia umaarufu mkubwa katika siku za hivi karibuni kufuatia kupinga kila hoja inayowasirishwa kwao.
Mjumbe mmoja aliyekataa kutaja jina lake kwa madai yeye si msemaji amedai kwamba kamwe uongozi wa Yanga hautathubutu kumpa ajira ya ukatibu mkenya huyo kwa vile si mwanayanga, ameongeza kupewa nyadhifa nyingine ikiwemo ujumbe si tatizo kwani ujumbe si mtu wa mwishoi kwenye maamuzi.
Amesisitiza kwamba wanataka katibu mkuu wa Yanga atoke kwenye kundi la wanachama wanaotambulika na si nje ya hapo, wameongeza kuwa kumleta mkenya ndani ya Yanga ni kukiuka katiba ya Yanga ambayo inaagiza wanachama tu ndio wanaopaswa kuongoza Yanga.