come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA KANYAGA TWENDE, SIMBA KUKALIWA KOONI NA MTIBWA!

Kivumbi cha Ligi Kuu Bara kinaendelea tena leo kwa timu zote 14 kushuka kwenye viwanja saba vya mikoa tofauti kusaka pointi tatu muhimu kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa huo.


Ligi hiyo ilikuwa imesimama kwa muda kupisha mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Brazil mwaka 2014, kwa timu za taifa.

Hata hivyo, macho na masikio ya mashabiki, wadau wengi wa soka nchini yatakuwa kwenye viwanja vya Taifa, Dar es Salaam na Sokoine, Mbeya.

Yanga, ambao ni mabingwa watetezi wanacheza na timu mpya yenye hamasa kubwa ya mashabiki mjini Mbeya, Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine huku Simba

ikiwa nyumbani jijini Dar es Salaam dhidi ya timu tishio, Mtibwa Sugar.

Yanga inatoka nje ya uwanja wake wa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu huku Simba ikirejeaa nyumbani kwa mara ya kwanza.

U/TAIFA, DAR ES SALAAM

Simba ambayo iliweka kambi yake Uufukweni Bamba Beach, Kigamboni, nje kidogo ya jiji ikijifua inacheza na Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mechi zote mbili za msimu wa ligi uliopita.

Mtibwa ambayo iliifunga Simba nyumbani na ugenini imetamba kurudia ubabe wa msimu uliopita, jambo ambalo linaongeza chachu, ushindani kwenye mechi hiyo.

Kocha Abdallah Kibadeni ‘King’ ameliambia gazeti hili jana kuwa: “Mtibwa ni timu kubwa, ina wachezaji wazuri, lakini vijana wangu wamejiandaa vya kutosha kukabiliana nao kwa kila hali. Natarajia ushindi wa kishindo. Kiufundi, tupo vizuri

na mbinu sahihi za kuwafunga Mtibwa.”

Naye kocha wa Mtibwa, Mecky Maxime alisema: “Tutacheza mpira wa akili ili kutimiza azma yetu ya ushindi. Nafikiri tutacheza mechi hiyo kwa kujiamini zaidi kwa vile