Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, zao lingine la kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji, alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya England na kufunga mabao mawili yaliyomfariji kocha David Moyes kwa ushindi wa 2-1.
Na wakati mkataba wa mshambuliaji huyo unamalizika miezi nane ijayo, klabu kadhaa zimeonyesha nia ya kumsajili, hivyo kocha huyo United anataka kumbakiza nyoa wake huyo mpya.