come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NIYONZIMA KUUPELEKA MOTO WAKE KAGERA.....

Baada  ya kuwa nje ya uwanja kwa wiki nzima, kiungo wa kimataifa wa Yanga Haruna Niyonzima 'Fabregas' amerejea kwenye kikosi cha 'Wanajangwani' kinachojiandaa kwa mechi ngumu ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar itakaopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Kocha msaidizi wa Yanga, Felix Minziro alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa nyota huyo wa Rwanda atacheza mechi ijayo dhidi ya Kagera.

Niyonzima ambaye aliukosa mchezo uliopita walioshinda 2-0 dhidi ya mabingwa wa Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar kutokana na matatizo ya kifamilia, jana alifanya mazoezi na wachezaji wengine wa Yanga kwenye uwanja wa shule ya sekondari Loyola uliopo Mabibo, Dar es Salaam.

"Hatuko tayari kupoteza pointi kwa sasa. Tunapeleka kikosi kizima Kagera," alisema Minziro.

Niyonzima aliunguliwa na nyumba yake wiki iliyopita na baadhi ya vitu vyake vya thamani kuteketea moto. Hakuna aliyedhurika katika moto huo.