come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TUTAICHINJA MAPEMA KAGERA SUGAR-BRANDTS

Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga Ernie Brandts, ametaja sababu tatu za kuiua mapema Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kesho.


Akizungumza na Kabumbu Spoti Brandts amesema kuwa Yanga itashinda mchezo huo ili kuipa presha Simba ambayo watakutana nanyo wiki ijayo, aidha Brandts ametaja sababu tatu za kuifunga Kagera ambapo ameweka bayana kuwa lengo kubwa ni kulipa kisasi.

'Sababu ya kwanza tunataka kulipiza kisasi baada ya kufungwa msimu uliopita katika uwanja huu wa Kaitaba, pili tunataka pointi tatu muhimu kila mechi, na mwisho kuwapa presha mahasimu wetu Simba ambao wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi tatu dhidi yetu', alisema kocha huyo.

Kikosi cha Yanga kiliwasili mjini Bukoba jana kikitokea Dar es Salaam ambapo kilicheza na Mtibwa Sugar wikiendi iliyopita na kuifunga magoli 2-0, ikicheza na Kagera kesho Yanga itaingia kambini kujiandaa na mechi nyingine ngumu dhidi ya hasimu wake mkuu Simba Jumapili ijayo katika uwanja wa Taifa.