Baada ya kuripotiwa kuwa ametibuana na kocha wake, Ernie Brandts kiasi cha kususia mazoezi, beki wa kutumainiwa wa Yanga, Kelvin Yondani na nyota wenzake 20 wa timu hiyo jana walitua kwa ndege mkoani Kagera kwa ajili ya mechi yao ya kesho ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji wao Kagera Sugar.
Yondani alikuwa katika msafara wa jumla ya watu 33 (pamoja na viongozi na benchi la ufundi) wa Yanga waliowasili Kagera saa 5 asubuhi jana kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Felix 'Minziro' alisema Yondani ni miongoni mwa wachezaji walioambatana na timu na kukanusha taarifa za kuwapo mtafaruku baina ya beki huyo na kocha Brandts.
"Hakuna mzozo wowote uliojitokeza baina na Yondani na Brandts, ndiyo maana nakuambia beki huyo ni kati ya wachezaji 21. Hatujui taarifa hizi zina lengo gani dhidi ya klabu yetu, ila tupo shwari kabisa," alisema Minziro.
Taarifa za vyombo vya habari jana viliripoti kuwa beki huyo na Brandts walitibuana kiasi cha mchezaji huyo kuvua jezi na kususa mazoezi.
Hata hivyo, Minziro alisema hakuna kitu kama hicho na kusema wanaenda Kagera wakiwa kamili gado kwa ajili ya kuwakabili wenyeji wao huku wakilichukulia pambano hilo kama 'mtihani mgumu' kwao ili kuhakikisha wanapata ushindi.
Yanga walilala 1-0 katika uwanja huo msimu uliopita wakati Brandts akiiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kufuatia kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha wao Mbelgiji Tom Saintfiet, hivyo wanatarajiwa kucheza kwa tahadhari kesho.
Kikosi kamili katika msafara huo kinawajumuisha ni makipa Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul.
Mabeki ni Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kelvin Yondani, huku viungo wakiwa ni Haruna Niyonzima, Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na Saimon Msuva.
Safu ya ushambuliaji ina Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi na Abdallah Mguhi 'Messi'.
Salum Telela na Bakari Kondo ni baadhi ya wachezaji walioachwa jijini Dar es Salaam, alisema meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh.
Aidha, alisema onyesho hilo linaloratibiwa na EATV na Radio, na kudhaminiwa na Vodacom, linatarajiwa kuwa la kihistoria kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, kwani ni mara ya pili kwa P-Square kuja Dar.