Timu ya Manchester City imeiadhibu Tottenham kwa jumla ya mabao 6 - 0 katika mechi ya kukata na shoka iliyochezwa siku ya jumapili.
Man City wakiwa nyumbani waliandika bao la kwanza katika sekunde ya 14 kwa goli safi lililotiwa wavuni na Jesus Navas.
Baada ya goli hilo Man City walicheza kwa kujiamini na kuifanya Tottenham wapoteane na ndipo katika dakika 34 Sandro wa Tottenham kutoka na makosa ya kipa wake Hugo Lloris kushindwa kuokoa shuti lililopigwa na Alvaro Negredo shuti hilo lilimgusa na kuingia wavuni.
Baadae Sergio Aguero kabla ya mapumziko akapachika bao la tatu hadi timu zinakwenda mapumziko Man City walikuwa mbele kwa magoli 3 - 0.
Kipindi cha pili timu zote ziliingia zikijaribu kujipanga lakini bado Man City walionekana kuutawala mpira na ndipo Sergio Aguero kwa mara nyingine akapachika goli akifuatiwa na Alvaro Negredo kabla ya Jesus Navas kukamilisha sherehe na kuizamisha Tottenham kwa jumla ya 6 - 0.
Kwa upande wao Manchester United wao walibanwa mbavu na Cardiff timu iliyoingia msimu huu kwenye ligi ya kuu ya England mechi iliyopigwa siku ya Jumapili baada ya kutoka sare ya magoli 2 - 2.