come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ALONSO KUTUA SUNDERLAND.

Sunderland wamefikia makubaliano ya kusaini hadi mwisho wa msimu mlinda ngome wa Fiorentina, Marcos Alonso kwa mkopo.

Alonso, ambaye alisakata kabumbu ya Ligi ya Premier awali na Bolton, alikamilisha mtihani wa kiafya na Sunderland Jumatatu na atajiunga na wenzake wakati dirisha la uhamisho litakapofunguka Januari.

Mchezaji huyo wa asili ya Uhispania, 23, atakuwa kiungo wa kwanza kusaini wa meneja Gus Poyet aliyerithi Paulo Di Canio Oktoba.

“Natoa idhibati kuwa Marcos atakuwa nasi hadi kilele cha musimu na ni jambo muhimu sana. Nilikuwa ninasaka mchezaji katika kitengo hicho upande wa kushoto na ninatumahi atatusaidia na kila mmoja atafurahia,” Poyet aliongezea.


Alonso alianza mchezo wake Real Madrid kabla ya kujiunga na Bolton na kufunga mabao tano kwenye mechi 35 kisha akahamia Fiorentina, pale ambapo ametoswa uwanjani mara tatu pekee.

Kilabu hicho cha Serie A ya Italia kilimuidhinisha kuhama Januari.