come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BEKI YANGA AKANUSHA KUCHEZA KWA DEIWAKA JANGWANI.

NAHODHA wa kikosi cha Young Africans U-20 ambaye pia msimu huu amepandishwa katika kikosi cha kwanza Issa Rashid Ngao amesema ameshangwaza na taarifa zilizotolewa jana katika baadhi ya mitandao kwamba yeye hana mkataba na Yanga na kusema hizo ni taarifa za uongo.

Ngao ambaye katika mashindano ya Uhai Cup yaliyomalizika mwishoni mwa wiki aliibuka mchezaji bora wa mashindano hayo amesema anashangazwa na taarifa hizo ambazo hazina ukweli wowote na kwamba yeye ni mchezaji wa Yanga kwa mkataba ndio maana analipwa haki zake kila mwisho wa mwezi.

Kiukweli hata mie nashangaa, sijui habari hizi hata wamezitoa wapi, hawajaongea na mimi kuweza kupata ukweli lakini cha ajabu hata hawakuweza kuwauliza viongozi wangu.

"Mimi ni mchezaji wa U20 Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili, nilisajiliwa siku moja pamoja na wachezaji wenzangu Rehani Kibingu, George Banda, Yusuph Abdul, Notikely Masasi na Mwinyi Bakari na wegine wengi tu"alisema Ngao.

Aidha Afisa Habari wa klabu ya Young Africans Baraka Kizuguto amesema ameshangwazwa na taarifa hizo ambazo hazijafanyiwa upembuzi akinifu kabla ya kutolewa kwa jamii, ukweli ni kwamba wachezaji wote Yanga wana mikataba na wanalipwa haki zao kila mwezi.


Hakuna mchezaji anayecheza bure Yanga wala bila kuwa na mktaba na kama kuna wanaojidanganya hivyo basi imekula kwao, vijana wote wa timu ya U20 wanatambulika na viongozi kwa ngazi zote kutokana na kutambulika kwa ajira zao ndani ya Yanga.

Issa Rashid Ngao pamoja na kuwa ni mchezaji wa timu zote za Yanga ya wakubwa na vijana U20, pia anaendelea na masomo katika chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es salaam akisomea Bachelor of Arts in Education  (BAE) akiwa mwaka wa pili sasa.