Nahodha wa Ghana, Asamoah Gyan, amesisitiza kwamba wameorodheshwa kwenye kundi kali zaidi kwenye Dimba la Dunia la Brazil 2014.
Ghana, maarufu Black Stars, wamejipata katika kundi moja na Ujerumani, Ureno na Marekani lakini nyota huyo anayesakata boli katika Milki za Kiarabu amesema wako tayari kukabiliana na yeyote.
“Kundi la Ghana ndilo gumu zaidi. Ni kundi la mauti,” Gyan alitangaza kwenye redio ya Asempa FM muda mfupi baada ya droo kufanyika Ijumaa.
“Lakini tuna kikosi kizuri kinachoweza kushindana na timu yeyote. Hakuna haja ya kuhofia Ujerumani, Ureno au Marekani.”
“Wananchi wa Ghana wanafaa kuwa watulivu, tutafuzu kutoka kundi hilo na kufanya kila mmoja wetu kupata shime tena.”
Droo kamili
Kundi A: Brazil, Cameroon, Mexico, Croatia
Kundi B: Uhispania, Chile, Australia, Uholanzi
Kundi C: Colombia, Cote d’Ivoire, Japan, Ugiriki
Kundi D: Uruguay, Italia, Costa Rica, Uingereza
Kundi E: Uswizi, Ecuador, Honduras, Ufaransa
Kundi F: Argentina, Nigeria, Iran, Bosnia Herzegovina
Kundi G: Ujerumani, Ghana, Marekani, Ureno
Kundi H: Ubelgiji, Algeria, Korea, Urusi