Mshambuliaji Mbwana Samatta wa Tout Poisant Mazembe (TP Mazembe) ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC meshindwa kuifikia rekodi iliyowekwa na mashambuliaji mwenzake wa timu hiyo Tresor Mputu ya kubeba mataji akiwa na timu hiyo.
Samatta amesahindwa kufanya hivyo baada ya timu yake ya TP Mazembe kushindwa kubeba ubingwa katika kipindi chake akiwa kama mshambuliaji tegemeo katika kikosi hicho kilichowahi kucheza fainali ya klabu bingwa ya dunia.
Mputu aliiwezesha TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Afrika mara mbili mfululizo pamoja na kuifikisha timu hiyo katika fainali ya klabu bingwa ya dunia, tofauti na ujio wa Samatta ambapo ameshindwa kuisaidia timu hiyo kutwaa angalau kombe la Shirikisho barani Afrika.
Hivi karibuni TP Mazembe imeshindwa kutwaa ubingwa wa kombe ka shirikisho baada ya kufungwa mabao 3-2 na timu kutoka Tunisia