come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

UKWELI UMENIONDOA SIMBA-KIBADENI.

Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba SC Abdallak Seif Athumani maarufu Kibadeni amedai tabia yake ya kusema ukweli dhidi ya wachezaji ndio imechangia kumuondoa katika kikosi cha wekundu hao waliokuwa katika vita ya kusaka ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Kibadeni amedai kusema ukweli kumemponza na kuondolewa katika benchi la ufundi la timu hiyo, lakini amejipa moyo na kuahidi kufanya kazi yake hatimaye kuinusuru timu yake mpya ya Ashanti United maarufu kama wauza mitumba wa Ilala.

Akizungumza na STAA WA LEO jana, Kibadeni aliyesaini mkataba mpya wa kuinoa timu hiyo amesema kuwa kitendo chake cha kusema ukweli kuwa Simba haina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu pamoja na kuwaweka sawa wachezaji wenye nidhamu mbaya klabuni ndio sehemu iliyochangia yeye kutupiwa virago.


'Mimi ni kocha na msimamizi wa wachezaji, najua kila mchezaji anavyocheza na nidhamu yake uwanjani na nje ya uwanja, napaswa kulalamika endapo tu nitakapoona inafaa kufanya hivyo, kusema ukweli nidhamu katika kikosi cha Simba imeshuka na unaona sasa hivi wanalumbana', alisema na kuongeza.

'Kuanzia wachezaji hadi viongozi hawashauriki, matatizo kila kukicha, Ashanti naweza kufanya kazi yangu kwa uhuru tofauti na Simba ambapo migogoro ilichukua nafasi', alilalamika kocha huyo mkongwe aliyewahi kuifikisha fainali ya kombe la CAF Simba mwaka 1993.