come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

WAISLAMU WAPANGA KUMSHITAKI LADY JAYDEE.

WIMBO wa Yahya uliotungwa na kuimbwa na mwanamuziki mahiri nchini Judith Wambura maarufu Lady Jaydee na kupokelewa vema na wapenzi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya sasa umesababisha balaa kwa mwanamuziki huyo kufuatia waumini wa dini ya Kiislamu kutaka kumshitaki kwa mwenyezi mungu kufuatia kulidhalilisha jina la Yahaya.

Mmoja kati ya waislamu waliopanga kumsomea dua baya msanii huyo kwa mwenyezi mungu ambaye amekataa kutaja jina lake ameiambia Staa wa Leo kuwa kitendo cha mwanamuziki huyo kulidhalilisha jina la Yahaya ni uchokozi mwingine kwa waislamu.

Muumini huyo maarufu kabisa katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni amedai Lady Jaydee amewadhalilisha waislamu hasa wenye majina ya Yahaya, pia amemdhalilisha mmoja kati ya manabii wa mwenyezi mungu, muumini huyo amemtaja nabii Yahaya ambaye alikuwa nabii wa mungu kwa ulimwengu kama walivyo manabiii wengine.


Amesema kuwa watu wanaoitwa majina ya Yahaya wameshuka hadhi na heshima, lakini jina la Yahaya ni la waislamu ni bora msanii huyoi angetumia jina lingine ambalo halipo katika imani ya dini yoyote huenda lingeleta ladha na ujumbe.

Ameongeza kuwa hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kuwakashifu waislamu katika nyimbo zake ambapo mara ya kwanza alimuimba Hassan katika wimbo wake wa 'Wanaume kama bunge', hata hivyo muumini huyo hajataja siku wala saa ya kumsomea dua baya staa huyo wa muziki wa kizazi kipya anayetamba na songi lake la Yahaya.

Mtandao huu ulikiri kupokea shutuma kadhaa kutoka kwa baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu kuupinga wimbo wa Yahaya kwa madai unawadhalilisha waislamu wenye kutumia jina hilo pia kumtusi nabii Yahaya.