Kiungo wa Serbia, Nemaja Matic, amerejea tena klabu cha Chelsea kwa makubaliano ya miaka mitano na nusu kutoka timu ya Ureno ya Benfica.
Taarifa iliyowasilishwa kwa soko la hisa la Lisbon ilidhibitisha kuwa vilabu vyote vilikuwa vimeafikiana Benfica watapokea Euro milioni 25 ili Chelsea wamiliki Matic kwa mara ya pili.
Baada ya kuwasili kutoka MSK Kosice mwaka wa 2009, Matic alitumika mara tatu kutoka benchi kabla ya kuaga Chelsea Januari 2011 kwa sehemu ya makubaliano yaliyomleta mlinda ngome David Luiz kutoka Benfica.
“Nimerithika sana na nafasi ya kurudi klabu hiki. Najihisi vizuri na lengo langu ni kuchezea Chelsea kadri ya uwezo wangu kurithisha mashabiki,” Matic alisema.
Meneja wake, Jose Mourinho, pia alielezea kunogeshwa kwake na Matic kurejea tena Stamford Bridge.
“Amenawiri kama mchezaji Ureno na ameibuka kama kiungo kigezo. Nina uhakika atakuwa nguzo muhimu ya kikosi na atachangia kuafikia malengo yetu,” Mourinho alizidi.