Timu ya Moyes imekumbana na mwanzo mbaya wa Mwaka Mpya lakini ilikuwa imefanikiwa kushinda mara nne, kutoka sare mara moja na kushindwa mara mbili pekee kwenye mechi saba za ligi mwishoni mwa 2013.
Raia huyo wa Scotland ameorodheshwa pamoja na meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini, ambaye hakushindwa Desemba, Jose Mourinho na Roberto Martinez wa Everton.
Chelsea walishinda mara tano kwenye mechi saba, wakatoka sare moja na kushindwa mara moja huku Martinez, aliyerithi Moyes Everton, akiongoza vijana wake kushinda mara nne katika mechi sita, kutoka sare moja na kushindwa moja.
United walianza mwezi Desemba kwa sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham kabla ya kushindwa nyumbani 1-0 na Everton na Newcastle.
Baada ya hapo, walishinda mara nne, dhidi ya Aston Villa, West Ham, Hull na Norwich, kabla ya kushindwa 2-1 nyumbani dhidi ya Tottenham Siku ya Mwaka Mpya.
Swansea walibandua United kutoka kwa Kombe la FA Jumapili kabla ya Sunderland kuwachapa 2-1 kwenye mechi ya kwanza ya nusufainali yao ya Kombe la Ligi.
Ni mara ya kwanza tangu 2001 kwa United kushindwa mechi tatu mfululizo.