Wajumbe wa Korea Kaskazini na Kusini wakati wa mkutano wa kuziunganisha familia
Korea Kaskazini na Kusini
zimekubaliana kuandaa shughuli ya kuwakutanisha watu wa familia
zilizotenganishwa na vita vya Korea miaka sitini iliyopita. Shughuli
hiyo itaandaliwa baadaye mwezi huu. Tangazo hilo limetolewa baada ya
mazungumzo ya haraka yaliyofanyika baina ya Korea hizo mbili katika
kijiji cha mpakani cha Panmunjom.
Zaidi ya familia watu alfu 70,000 waliopoteana na jamaa zao wanaishi Korea Kusini na wengi wao kwa sasa wana umri wa zaidi ya miaka 80.
Raia wa Korea Kusini wanaosubiri kukutana jamaa zao wa Kaskazini
Rais Wa Korea Kusini alielezea umuhimu wa kutekeleza zoezi hilo la kuunganisha jamaa za watu hao katika hotuba yake ya mwaka mpya. Na mwezi uliopita, Korea Kaskazni ilianza kuisihi Kusini kukomesha vitendo vya uhasama lakini wengi hawaamini kama uhusiano mzuri utaweza kupatikana kwa urahisi.
Mwandishi wa BBC aliyepo mjini Seoul anasema zoezi la kupatanisha familia hizo lilifutiliwa mbali na Korea Kaskazini na huku mazoezi makubwa ya kijeshi yakitarajiwa kuanza Korea Kusini baadaye mwezi huu, wengi wanajiuliza iwapo hali ya kuimarisha uhusiano kwa sasa itadumu.