TIMU
ya Real Madrid imetanguliza mguu mmoja katika Fainali ya Kombe la
Mfalme kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhid ya Atletico Madrid katika Nusu
Fainali ya kwanza Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mabao
ya Real yalifungwa na Insua aliyejifunga dakika ya 17, Jese dakika ya
57 na Di Maria dakika ya 73. Sasa Real inaweza ikakutana katika Fainali
na wapinzani wao wakubwa Hispania, Barcelona ambao nao pia jana
waliifunga 2-0 Real Sociedad.
Cristiano Ronaldo akionyesha mavitu yaliyompa Ballon d'Or winner
Pepe akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid jana