Yanga imepanga kuvuna Sh253 milioni katika mchezo wao na Komorozine ya Comoro huku mchezaji wake Athuman Idd Chuji akipigwa Stop kuichezea timu hiyo.Klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani itavuna fedha hizo ikiwa ni mapato ya mlangoni yatakayopatikana baada ya kuuza vitabu vya tiketi 45,000, ambapo kingilio cha juu kabisa katika mchezo huo ni Sh30,000 na kingilio cha chini ni Sh5,000.
Yanga itashuka dimbani keshokutwa Jumamosi kumenyana na’Komorozine ya Comoro ambayo imetua nchini jana.