|
|
Licha ya klabu chake Chelsea kufungua mwanya wa
alama saba uongozini wa ligi ya Premier ya Uingereza, meneja wa timu
hiyo, Jose Mourinho, amesema angependelea kuwa katika nafasi ya
Manchester City katika harakati za kuwania taji hilo.
Chelsea walibwaga Tottenham Hotspurs 4-0 na kuzoa alama 66 huku Liverpool na Arsenal wakifuata na alama 59 ingawa wamecheza mechi moja chache.
City wamo alama mbili nyuma ya wawili hao lakini Chelsea wamecheza mechi tatu zaidi na pia wana ubora wa mabao na hilo limesababisha Mourinho kudai kuwa vijana hao wa Manuel Pellegrini wana uwezo mkubwa kunyakua taji la Premier.
“Ningelitaka kuwa katika nafasi yao. Wakishinda mechi walizo salia nazo mkononi, watakuwa viongozi wa ligi. City wakishinda mechi zote 12 zilizosalia, basi watakuwa mabingwa. Hatima yao iko mikononi mwao,” Mourinho alibeza.
Meneja huyo alikiri kuwa Chelsea wametimiza lengo lao la kuhakikisha watakuwa miongoni mwa nne bora katika shindano hilo baada ya kusonga alama 13 mbele ya Tottenham wanao miliki nafasi ya tano.
“Sisi wenyewe ndio tunaweza poteza kuorodheshwa kati ya nne bora. Tuko alama 13 mbele ya Tottenham na 15 mbele ya Man United na Everton. Sidhani tunaweza pokonywa hadhi hii sasa.
“Sasa lengo letu ni kumaliza katika nafasi tatu za kwanza kuhakikisha kufuzu kombe la Champions League moja kwa moja,” mwalimu huyo aliongeza.
Samuel Eto’o aliwapatia Chelsea uongozi kabla ya kukejeli tetesi za Mourinho kuhusu umri wake halisi huku akiiga mkongwe kwa kujidai anatembea na mkongojo baada ya dakika 56 kutimia.
“Sikumshawishi asherehekee bao lake hivyo lakini tulijua litatendeka. Tulionelea hilo linafaa. Kukejeli ni vyema kwani linasitisha swala hilo,” Mourinho aliongeza.
Eden Hazard aliziba penalti wavuni baada ya Eto’o kuangushwa na Younes Kaboul ambaye alikula nyekundu dakika tatu baadaye kabla ya mshambuliaji Demba Ba kutoka kwenye benchi na kufunga mawili yaliokamilisha udhia.