Matokeo hayo yanaifanya Simba SC ijiongezee pointi moja na kufikisha 36 baada ya kucheza mechi 21, ikiendelea kubaki nafasi ya nne, wakati Prisons imetimiza pointi 22 baada ya mechi 20 na inabaki nafasi ya 10.
Mchezo ulikuwa mkali na wa upinzani mkali kiasi kwamba beki Nurdin Issa Chona wa Prisons aligongana na mshambuliaji wa Prisons, Amisi Tambwe kipindi cha kwanza na kuumizana kiasi cha kila mmoja kufungwa bandeji kubwa ya kuzunguka kichwa.
Tambwe alipasuka kisogoni na kutolewa nje kwa machela kabla ya kurejea uwanjani, wakati Chona alijivuta mwenyewe nje akisaidiwa na Daktari wa Prisons baada ya kupasuka kwenye paji la uso.
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam JKT Ruvu imeilaza Mtibwa Sugar mabao 2-1, yaliyotiwa kimiani na Hussein Bunu dakika ya 39 na Amos Mgisa dakika ya 75, wakati bao la Wakata Miwa wa Manungu lilifungwa Vincent Barnabas dakika ya 70.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Yaw Berko, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo/Betram Mombeki dk46, Henry Joseph/Said Ndemla dk82, Amri Kiemba, Amisi Tambwe na Ramadhani Singano ‘Messi’/Ali Badru dk70.
Prisons; Beno Kakulanya, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, Jumanne Fadhil, Lugano Mwangama, Nurdin Issa, Freddy Chudu, Omega Seme/Jimmy Shoji dk88, Peter Michael/Brighton Mponzi dk86, Frank Hau na Sixbert Mwasekaga.