come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA WAAPAKUING'OA AL AHLY

Na Mwandishi wetu Cairo

MABINGWA wa soka Tanzania bara na wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa Yanga wameapa kuing'oa mashindanoni mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa National Al Ahly ya Misri katika mchezo wa marudiano utakaofanyika siku ya jumapili huko Alexandria.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyepo Misri, Simon Msuva amesema wana kila ari na kasi kubwa kusonga mbele katika michuano hiyo na hatimaye juitoa mashindanoni Al Ahly, Msuva ameendelea kwa kusema Al Ahly ni timu ya kawaida sana isipokuwa ina wachezaji wazuri.

Naye Mrisho Ngasa amesema ataendeleza moto wake wa kucheka na nyavu ili kuhakikisha Yanga inasonga mbele, 'Tuna timu nzuri hivyo tujitahidi angalau tuweze kuwafurahisha Watanzania', alisema na kuongeza, Al Ahly ni timu bora lakini na sisi ni bora na ndio maana tukawafunga nyumbani bao 1-0', alisisitiza.


Beki wa kati wa timu hiyo Kelvin Yondani amedai yeye kazi yake ni moja tu kuhakikisha washambuliaji wa timu hiyo hawaendi kokote, naye kocha msaidizi wa Yanga Cherles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kikotayari kwa vita na lolote linaweza kutokea