come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DK RAJABU AELEZEA WACHEZAJI NA WANAMUZIKI MAARUFU WANAVYOMIMINIKA KWAKE KUFUATA DAWA

JANA Jumamosi tumeshuhudia burudani safi na ya kupendeza, ambapo historia imewezwa kuandikwa katika tuzo za Kilimanjaro Muzic Award kufuatia mwanamuziki maarufu Diamond Platinum kuchukua tuzo saba mfululizo.

Leo hii kutakuwa na burudani nyingine ambapo timu ya taifa, Taifa Stars itakuwa na kibarua pevu pale itakapombana na timu ya taifa ya Malawi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mchezo huo ni wa kirafiki, juma lililopita wakati Tanzania kisherehekea muungano wake wa miaka 50,Stars ilifungwa na Burundi mabao 3-1 hivyo mchezo wa leo unaweza kuturudisha tena machungu Watanzania ambao jana walikuwana furaha pale Mlimani City wakati utolewaji wa tuzo ulipofanyika.

Ushindi wa Diamond ulipokelewa kwa furaha na vigeregere na wapenzi na mashabiki wake, kule jijini Mbeya timu ya soka ya taifa, Taifa Stars ilionyeshana kazi na Malawi.


Tuachane na hayo, kufuatia kushamili kwa matukio yakishirikina kwenye mchezo wa soka na muziki pia, safu hiiilifanya mahojiano na mganga wa tiba asilia anayesifika kwakutibu maradhi mbalimbali ambaye pia ni mtabiri wa mechi za soka duniani.

Dk Rajabu Kondo mwenye maskani yake Bunju B nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ameweka hadharani kuwa baadhi ya wanasoka nchini pamoja na wanamuziki wamefuata huduma yake mara kwa mara.

Mganga huyo anayetumia uchawi asilia amedai uchawi upo michezoni, 'anayetaka kupinga kuwa uchawi hakuna mwache abishe lakini ukweli uliopo uchawi upo na mimi nimeshawapokea wacheaji wa timu kubwa ili niwagange', alisema na kuongeza.

'Kwenye vilabu vikubwa mambo ya kishirikina yamekithili, kuna wachezaji wengine wanatum,ia ndumba ili wapate namba ya kudumu bila kujali kiwango chake, mwalimu atampanga tu kwa sababu ndumba inafanya kazi yake', aliendelea.

'Na wateuzi wa timu ya taifa watavutiwa naye hata kama kiwango chake ni kidogo, mashabiki nao watampenda, huo ni uchawi hatari sana ambao mimi kwangu upo na nimeshawapa wachezaji wengi na wamefanikiwa', alisema.

Ingawa amekataa kuwataja kwa madai ni wateja wake na asingependa kuwatolea siri, 'nimeshasaidia ushindi wa timu  mbalimbali hapa nchini na nyingine zikapanda daraja, na zile za mitaani usiseme watu wengi wamenifuata na kuwawezesha kuchukua makombe ya ng'ombe, mbuzi na jezi', aliendelea Dk Rajabu.

Akielezea historia yake ya uganga, Dk Rajabu anasema alianza kujishughurisha na kazi hiyo tangia mwaka 1961 ambapo alifafanua kuwa aliachiwa na marehemu baba yake, aliendelea na kazi hiyo na kujikuta anafanikiwa kuwatibu watu wengi na sasa amegeuka mtabiri wa mechi za ligi kuu mbalimbali duniani.

Dk Rajabu ni mtaalamu kutibu magonjwa sugu na alilowea zaidi Sumbawanga ambapo ndipo alipoanza shughuri hiyo kwa kutoa tiba na kuwaponya watu, alisafiri mikoa mbalimbali ya nchi kabla hajachukuliwa na Mtanzania mmoja mwenye asili ya Asia ambapo alikwenda naye Dubai.

Alipokuwa Dubai, Dk Rajabu alifanikisha matatizo ya watu huko ambapo kulikuwa na mwarabu mmoja alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa mtindio wa ubongo yaani alikuwa na kichaa, lakini kwa maajabu yake alifanikiwa kumponya maradhi hayo.

Kwa sasa ana uhakika mkubwa wa kumtibu mtu mwenye kichaa pamoja na mtu aliyepatwa na kiharusi (Kupararaizi) akielezea jinsi ya kusafisha nyota za watu mbalimbali, Dk Rajabu anasema wasanii wengi hapa nchini amekuwa akiwang'arisha nyota zao na kufanikiwa.

'Kuna idadi kubwa kati ya wasanii niliowapa kinga na kusafisha nyota zao, idadi ni kubwa ila siwezi kumtaja mmoja mmoja wenyewe wanajielewa, pia nimesafisha nyota za wacheaji wengi tu mastaa ambao walififia hivi karibuni, lakini walipofika kwangu kusema kweli mambo yao yamenyooka', alisema.

Mganga huyo amedai lengo lake ni kutokomeza uchawi unaotegwa na watu wenye nia mbaya hivyo anaweza kusafisha uchafu huo kwa kutumia kalama yake aliyopewa na mwenyezi mungu.

Amedai tiba asilia ilithibitishwa na mungu na aliwataka wanadamu wake kuitumia pindi wanapopatwa na matatizo, tembelea tangazo lake)

Mwandishi wa safu hii alimuuuliza Dk Rajabu kama anaweza kuisaidia Tanzania kufuu fainali za mataifa Afrika mwakani endapo atafuatwa na shirikisho la kandanda nchini TFF, DK Rajabu alisema uwezo huo anao kwani kwa sasa Tanzania imefunikwa na wingu jeusi na ndio maana imekuwa ikishindwa
katika michezo yote.

'Tanzania imefunikwa na wingu jeusi na ndio maana kila inapotokea mashindano tumeishiwa kutolewa, lakini mafanikio yanaonekana, TFF wanifuate tu nikomeshe uchawi huo, unajua wenye kusababisha yote nawajua', aliongeza.

Aidha Mganga huyo amewataka watu wenye matatizo mbalimbali kama kifafa, uchizi, pumu, uzazi kwa mwanaume na mwanamke. kupalalaizi, matego ya shamba na nyumba, kusafisha nyota,
kupandishwa cheo kazini, mvuto wa biashara, kutoa vitu vibaya mwilini, nguvu za kiume, vidonda vyatumbo pamoja na waandaaji wa ligi za soka kuna dawa yao ya kutega ili zisitokee vurugu nk.

Mganga huyo aliendelea kwa kusema kinga ya mwili ni kitu muhimu ambapo amedai anazo dawa za kuimarisha uhai wa mtu, safu hii iliondoka maeneno ya Bunju B ikiwa na maswali kadhaa ambapo Dk Rajabu alituachia, Ni kweli uchawi unazuilika? ni jambo la kusubiri kisha tuone

Dk Rajabu anapatikana kwa namba 0712 666487/0657 887760 na 0688 904777, waweza kufika ofisini kwake Bunju B nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.