MSANII chipukizi wa miondoko ya hiphop Robert Michael ameomba msaada wa fedha ili aingie studio kurekodi nyimbo zake alizotunga hivi karibuni, akizungumza na mwandishi wa habari hizi Michael amedai muziki upo ndani ya damu yake lakini amekosa fedha za kumwezesha kuingia studio.
Anasema tangia amalize masomo yake ya kidato cha nne bado hajapata kazi ya kumwezesha apate pesa hivyo ameamua kuufanya muziki kuwa ajira yake, amewwataka watu wenye moyo kumsaidia ili aweze kutengeneza kazi yake na kujipatia kipato.
Michael amedai muziki ni ajira kwani vijana wengi wameweza kunufaika kupitia muziki, hivyo na yeye anataka kuonyesha kuwa kipaji chake alichoojaliwa akiwezi kupotea, tayari msanii huyo ametunga nyimbo mbili ambazo ni 'ugumu wa maisha' na vumilivu.
Endapo mtu mwenye moyo atajitokeza basi ampigie kwa namba ya simu 0752 059085
