BAADA ya kuondoka kwa wachezaji wawili wa kutumainiwa katika kikosi cha Yanga Mrundi Didier Kavumbagu na mzalendo Frank Domayo, wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga wameelekeza nguvu zao kwa wachezaji wao Jerry Tegete na Salum Telela ambao tayari wapo fiti kuitumikia Yanga kwa moyo mmoja msimu ujao.
Tegete na Telela wametajwa kama wachezaji muhimu katika kikosi hicho kwakuwa baada ya kuumia ndio kuliwqapa fulsa Domayo na Kavumbagu kuanza katikakikosi cha kwanza, Zaituni Mrapi mpenzi na shabiki wa Yanga amesema anaukumbuka mchango wa Telela katika kikosi cha Yanga tofauti na Domayo ambaye alishindwa kuisaidia Yanga licha ya kuonyesha kiwango chale.
'Telela aliifungia Yanga goli muhi9mu tulipocheza na Azam ambapo tulishinda 1-0 kwenye Ngao ya Hisani mwaka jana, naye Tegete alikuwa akimuweka benchi Kavumbagu mpaka alikuwa akilalamika kuwa anarogwa wakati ukweli usiopingika Tegete yuko juu zaidi yake', alisema shabiki huyo.
Kuondoka kwa nyota hao wawili kumeweza kuleta chokochoko ndani ya Yanga kiasi kwamba baadhi ya mashabiki wameandamana hadi kwa aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Yanga Davies Mosha huku wakiupinga uongozi wa Yanga uliopo madarakani unaoongozwa na Bilionea Yusuf Manji