come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA YAANDAA MIKAKATI MIZITO KUZIBOMOA SIMBA. AZAM

Yanga  tayari wameungana na sasa wanaandaa mikakati mizito kuzibomoa Simba na Azam ambazo zimetangaza vita dhidi yake, Azam imeshaanza vita hivyo kwa kuwasainisha nyota wake wawili Mrundi Didier Kavumbagu na mzalendo Frank Domayo huku ikimuwinda vikali beki wake raia wa DRC Congo Mbuyu Twite.

Simba nayo imetangaza vita dhidi ya Yanga kwa kutaka kuwasainisha wachezaji wake Ally Mustapha 'Barthez', David Luhende na Athuman Idd 'Chuji'  ambao bado hawajatangazwa kuachwa, kwa taarifa hiyo uongozi wa Yanga umetangaza kuwatengea vitita nyota wa timu hizo mbili zenye mahusiano.


Kigogo mmoja wa Yanga anayesaifika kwa kufanya usajili wa kushtua ameiambia Staa wa Leo kuwa Yanga imepanga kuzibomoa Simba na Azam na wajiandae kulia, pasipo kutaja nyota gani inaotaka kuwachukua kigogo amesema watafanya ukatiri huo mwishoni mwa wiki hii.

Staa wa Leo inafahamu waziwazi kuwa Yanga inafanya mazungumzo ya siri kwa siri na wachezaji wawili wa Azam ambao mikataba yao iko ukingoni huku wengine wakitaka kuongezewa, nyota hao ni Gaudence Mwaikimba ambaye aliwahi kuichezea Yanga na Salum Abubakar 'Sure Boy'.

Kwa upande wa Simba mtandao huu unafahamu kuwa mshambuliaji raia wa Burundi Amissi Tambwe na kiungo mkabaji Jonas Mkude wapo mbioni kusajiliwa na Yanga kwa gharama yoyote huku kiongozi mmoja wa Simba akihusika katika usajili huo.

Tayari kiungo Henry Joseph ametangaza ofa kwa timu yoyote inayomuhitaji wakati Uhuru Seleman na kipa Yaw Berko wametemwa hivyo ni rahisi kujiunga na timu yoyote ile