Timu ya taifa ya Argentina imepokelewa kwa shangwe na maelfu ya watu waliotaka kuwapongeza wachezaji wao, kuanzia uwanja wa ndege.
Wanandinga hao walishuka kutoka kwenye ndege maalum iliyokuwa imenakshiwa kwa rangi za timu hiyo ikiwa na maandishi yaliyomaanisha 'Asante Argentina' kwa lugha ya kwao.
Dege hilo linatua na wachezaji wa Argentina ambao wameitoa kimasomaso nchi yao na kufika fainali baada ya miaka 24 tangia ilipofanya hivyo
Wachezaji hao walipita kwenye mitaa wakiwa ndani ya mabasi maalum huku kukiwa na mapokezi makubwa kuwahi kushuhudiwa.
Argentina iliingia fainali za kombe la Dunia 2014, na kushindwa kutimiza ndoto yao ya kutwaa kombe hilo kwa kufungwa na timu ya Ujerumani kwa bao moja.