come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BOB JUNIOR ADAIWA KURUDIANA NA MKEWE, MWENYEWE APATA KIGUGUMIZI KUJIBU

Juzi zilianza kusambaa upya habari kuwa Bob Junior amempa tena talaka mkewe Halima Ali ambaye ni muigizaji wa filamu baada ya kudaiwa kurudiana miezi kadhaa baada ya siku za nyuma kumpa talaka.


Siku za mwanzo inadaiwa muigizaji Ashley Toto anayeishi Ujerumani alikuwa akitoka kimapenzi na Bob Junior ndiyo sababu ya ndoa kuvunjika, na juzi ikadaiwa ndugu wa Bob Junior wanamuona Halima hana nyota angavu ikidaiwa Bob Junior anashuka kimuziki.

Alipoulizwa Bob Junior juzi kama ni kweli ameachana na Halima tena akajibu "Sikuwahi kurudiana na mke wangu nipo single tokea wakati huo"

Hata hivyo miezi michache zilisambaa picha zikimuonyesha Bob Junior na Halima wakiwa wamefunga ndoa upya na mtandao huu ulimuuliza Bob Junior na alikubali kuwa walirudiana kweli ila kwasasa jibu lake limezua utata.