come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MARKOVIC ATUA LIVERPOOL KUMALIZA MAMBO AWASAHAULISHE KUHUSU SUAREZ

MSHAMBULIAJI Lazar Markovic ataigharimu Liverpool Pauni Milioni 20 leo atakapothibitishwa kusajiliwa na kocha Brendan Rodgers.

Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Serbia aliwasili Merseyside Jumapili usiku kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya katika hospitali ya Spire Liverpool iliyopo viwanja vya mazoezi vya klabu, Melwood baada ya Liverpool kukubali kutoa Pauni Milioni 20 kumnunua kutoka Benfica.

Liverpool imekuwa ikimfukuzia kwa muda mrefu Markovic hata kabla Luis Suarez hajahamia Barcelona – na wanataka kufanya jithada za haraka kupata mshambuliaji hatari kinda Ulaya.


Markovic, ambaye alitoa mchango mkubwa kwa Benfica kutwaa taji la Ligi Kuu ya Ureno msimu uliopita, amekubali mkataba wa muda mrefu na ataungana na Rickie Lambert, Adam Lallana na Emre Can katika orodha ya wachezaji wapya wa timu hiyo iliyoshika nafasi ya pili Ligi Kuu England Mei mwaka huu nyuma ya Manchester City.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 hatakuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa Liverpool, kwani timu hiyo bado inawataka mshambuliaji wa Ubelgiji, Divock Origi na beki wa kushoto wa Sevilla, Alberto Moreno.