come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DIANA KIMARO AINGIA ANGA ZA MANAIKI SANGA, YULE MVULANA KIWEMBE KWA MADEMU WA KIBONGO

Sio siri tena ! Mastaa wa filamu nchini Diana Kimaro na Manaiki Sanga ni wapenzi. Juzi tulipenyezewa habari kuwa Manaiki anatoka na Diana Kimaro na kwasasa wameshibana vya kutosha kila mtu yupo hoi kwa mwenzake kama mlenda !.


Uzuri ni kuwa wakati tukipewa hot gossip hiyo Manaiki mwenyewe alikuwepo eneo hilo hilo ambapo wasanii kadhaa walikuwa wakifuturu pamoja hivyo haraka sana tukampiga swali la moto Manaiki kama ni kweli yeye na Diana kwasasa ni honey, sweet na mpenzi?

Manaiki alibaki kuangua kicheko ambacho kilitoa jibu la moja kwa moja kuwa hajiwezi kwa Diana ambaye kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo anavyozidi kujiimarisha kwenye tasnia ya filamu Swahiliwood.

Kiwembe huyu jamaa kwa watoto wa kike hasa wasanii wa bongomovie, sasa anachukua ngoma mbichi Diana Kimaro

Pia kupitia mitandao ya kijamii Manaiki amekuwa akiandika ujumbe na kupost picha akiwa na Diana.

moja wa ujumbe huo ni huu "#love #never #die japokua haupo na Mimi ila everyday mi naku feel baby sijuwi kupendwa kama we ulivyokua unanipenda na hiyo ni habari ya mjini"