Maafisa wa polisi nchini Brazil
wamemkamata afisa mkuu mtendaji wa kampuni mshirika wa FIFA kwa tuhuma
za uuzaji tiketi za kombe la dunia kinyume na kanuni.
Polisi walisema kuwa kikundi hicho kilikuwa sehemu ya genge kubwa la kimataifa ambalo lilikuwa likiuza tiketi ambazo zilikuwa zimetengewa makundi maaluma ikiwemo tiketi zilizokuwa zimetengewa wachezaji .
Kufuatia kashfa hiyo uchunguzi unaendelea kubaini iwapo baadhi ya tiketi hizo zimeuziwa watalii ambao hawakujua walikuwa wanakiuka sheria za shirikisho la soka duniani FIFA.
Kompyuta na vifaa vyengine vya kielektroniki vilikamatwa na polisi kwa uchunguzi zaidi kutopka kwa mkahawa huo wa kifahari ulioko Copa Cabana Palace Hotel
Afisa anayeongoza uchunguzi huo Fabio Barucke, amesema kuwa afisa huyo alikuwa na hati zinazomruhusu kuingia katika afisi zote za fifa kwa hivyo alikuwa na uwezo wa kuzipata tiketi hizo.