come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAKALA: NANI AKATWE KATI YA OKWI AU KIIZA?

NI suala gumu mno na zito kuamua nani asalie katika kikosi cha Yanga msimu ujao, vuguvugu la usajili ndilo lililoamua hivyo ambapo sasa klabu ya Yanga inataraia kuwasilisha majina matano ya wachezaji wa kigeni badala ya sita ilionao.

Yanga hadi sasa ina wachezaji wa kigeni sita wakati shirikisho la kandanda nchini TFF limeweka sheria zake ambapo wachezaji wa kigeni mwisho watano.

Endapo Yanga itapitisha majina ya wachezaji wa kigeni watano italazimika kumkata mchezaji mmoja, Yanga inao wachezaji sita wa kigeni kufuatia kusajili wachezaji wawili toka Brazil.


Yanga iliwasajili Andrey Coutinho anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na Genlison Santana Santos 'Jaja' ambaye ni mshambuliaji, hivyo wanaungana na Hamis Kiiza, Emmanuel Okwi, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima.

Kuna mapendekezo kadhaa yamewasilishwa na wadau mbalimbali wa klabu hiyo wakitaka mchezaji fulani akatwe, hiyo imekuja kufuatia Mbrazil Jaja kumwaga wino wa kuitumikia Yanga miaka miwili.

Lakini hivi karibuni taarifa nyingi zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Yanga inataka kumkata mshambuliaji wake mahiri Hamis Kiiza ambaye katika msimu uliomalizika aliifungia Yanga mabao 11 nyuma ya Mrisho Ngasa aliyefunga 12 Kiiza anatazamwa kwa macho matatu kuwa anastahili kuondoklewa katika kikosi hicho kutokana na kutoonyesha ushirikiano wa kutosha katika kikosi hicho, Kiiza ameshindwa kuisaidia Yanga kutetea ubingwa wake wa bara iliokuwa inaushikilia, ubingwa huo umechukuliwa na Azam FC.

Okwi anaonekana msumbufu mno hivyo anawezwa kukatwa katika kikosi cha Yanga 

Pia ameshindwa kuisaidia Yanga kuiondoa mashindanoni Al Ahly ya Misri katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, aidha ripoti ya mwalimu aliyemaliza muda wake Mholanzi Hans Van Der Pluijm ilitaka Kiiza atemwe.

Inadaiwa Kiiza ameshindwa kumpa ushirikiano wa kutosha mshambuliaji mwenzake Emmanuel Okwi na kupelekea kushindwa kuisaidia Yanga, kwa upande mwingine Yanga wanataka kumkata Okwi kwa sababu ni msumbufu.

Okwi ameonyesha nidhamu mbovu msimu uliopita kwa kushindwa kuitumikia timu yake katika mechi za mwisho wa msimu na kupelekea kikosi hicho kupokwa ubingwa, umuhimu wa Okwi ungeisaidia Yanga kufanya vizuri lakini akaingia zake mitini na kuanzisha malumbano yasiyo na hoja na uongozi.

Malumbano hayo yalitokana na madai yake ya pesa za usajili ambazo inasemekana alikuwa anaidai Yanga zaidi ya mil 64 za Kitanzania, hata hivyo Yanga ilimaliza ligi ikiwa katika nafasi ya pili na Azam FC ikitawazwa mabingwa wapya wa bara kwa mara yake ya kwanza.

Uongozi wa Yanga chini yake milionea Yusuf Manji uliingia katika malumbano na mchezaji huyo anayeripotiwa mara kwa mara kutaka kurejea klabu yake ya zamani ya Simba, pia usajili wa mchezaji huyo ulikuwa na mkanganyiko mkubwa uliopelekea TFF kutaka ufafanuzi kutoka Fifa ili kumruhusu kucheza ligi kuu ya bara msimu uliopita.

Umuhimu wa nyota hao:

Emmanuel Okwi anaonekana kuwa na umuhimu mkubwa katika kikosi cha Yanga, kwa usajili wa wachezaji wa kigeni Yanga imelamba dume kwa mchezaji huyo kwani anajua nini anachokifanya, ila Yanga inaweza kujuta kutokana na nidhamu ya mchezaji huyo aliyonayo.

Kuna fununu kuwa usajili wa Okwi ulikuwa wa kimagumashi na ukapelekea bosi wa Yanga kumuondoa katika kamati ya usajili aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo Abdallah Bin Kleb maarufu Al Mansoor.

Bin Kleb ametupwa nje katika kamati mmpya iliyotangazwa mapema wiki hii na bosi wa Yanga Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga, Okwi sidhani kama anaweza kuendana na kocha mwenye msimamo wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo.

Lakini Okwi anabaki kama mchezaji pekee na mwenye thamani wa kigeni wanaocheza soka la kulipwa hapa nchini, Okwi yuko juu ya Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu wa Azam FC, Amisi Tambwe na wengineo.

Hamisi Kiiza

Ni mshambuliaji makini aliyekuwa mwiba katika kikosi cha Yanga, Kiiza aling'ara mno katika mzunguko wa kwanza ambapo aliweza kufukuzana kwa mabao na Amisi Tambwe wa Simba ambaye aliibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu na kuchukua kiatu cha dhahabu.

Uwezo wake wa kufunga uliifanya Yanga ifukuzane na vinara Azam katika mbio za ubingwa, kama si bahati mbaya Yanga ingeweza kuwa mabingwa wa ligi kuu kwani ilikuwa na kikosi hatari mno, sina shaka na kiwango cha Kiiza katika upachikaji mabao.

Anasifika kwa kuitungua Simba mara mbili mfululizo, Kiiza alikuwa mfungaji wa bao la pili na la ushindi wakati Yanga inafunga Simba mabao 2-0, magoli ya Yanga yalifungwa na Didier Kavumbagu ambaye kwa sasa yupo Azam na la pili likifungwa na Kiiza.

Enapo Yanga itamkata Kiiza itakuwa imepata hasara kubwa, kwani magoli yake 11 aliyofunga msimu uliopita yalikuwa mengi zaidi kwenye mbio za ufungaji bora, alishika nafasi ya nne kwa ufungaji akiwa nyuma ya Elias Maguli Mrisho Ngasa na kinara Amisi Tambwe.

Yanga inawezaje kumkata straika anayefumania nyavu? basi ni hasara kubwa wanaweza kuipata,
nani akatwe kati ya Okwi au Kiiza kulingana na matakwa ya uongozi wa Yanga ebu jaribu kupiga kura yako kupitia namba hii 0755 522216.