

Kutoka Ligi ya Mabingwa hadi...

Bosi: Rafa Benitez akitabasamu wakati akiinua taji la Europa League Uwanja wa Amsterdam

Tabasamu: Frank Lampard

BAO la Branislav Ivanovic dakika ya pili ya muda wa nyongeza kati ya tatu baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, usiku huu limeipa Cheslea Kombe la Europa League baada ya kuilaza Benfica ya Ureno mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena.
Beki huyo wa Serbia, alipaa hewani kwenda kuufuata mpira wa kona uliopigwa na Juan Mata na kuujaza nyavuni.
![]() |
| Ivanovic akifunga bao la pili na la ushindi |
Katika mchezo huo, kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Lampard, Luiz, Ramires, Mata, Oscar na Torres.
Benfica: Artur Moraes, Almeida, Luisao, Garay, Melgarejo, Perez, Matic, Rodrigo, Gaitan, Cardozo, Salvio.


Pati la ubingwa: Branislav Ivanovic akipongezwa na wenzake

Ramires wa Chelsea akikabiliana na Lorenzo Melgarejo wa Benfica

Magwiji watatu: Eusebio, Michel Platini na Johan Cruyff wakiangalia mechi hiyo Amsterdam Arena

Gwiji na mwali: Patrick Kluivert akiwasilisha Kombe la Europa uwanjani




Mbata: Rodrigo wa Benfica akimpa mbata Cesar Azpilicueta wa Chelsea

Haikuwa bahati: Torres alichezewa rafu ya penalti, lakini refa akapeta

Tunamtaka Mourinho: Mashabiki wa Chelsea waliwasilisha hisia zao leo juu ya kocha atakayerithi mikoba Rafa Benitez


