Kwenye
mchezo wa mwisho wa kihistoria wa Alex
Ferguson mbele ya mashabiki zaidi ya 70000 ndani ya Old Trafford
aliamua kumcheza Paul Scholes na kumuacha Wayne Rooney katika timu yake
ya siku hiyo. Alisema kwamba alihisi akili ya Rooney ilikuwa sehemu
nyingine baada ya mara nyingine kuomba kuondoka Old Trafford. Ferguson
alisema amekataa ombi hilo na anaamini Rooney anahitaji muda tu
kufikiria kwa kina kuhusu uamuzi wake, lakini naamini Rooney ni tatizo
ambalo kocha mpya hahitaji.
Wayne
Rooney alikuwepo uwanjani huku akicheka na kufurahia na wenzie kwa
kuimba nyimbo za ushindi. Alionekana kuwa na furaha kabisa. Ulikuwa ni
ushangiliaji ule ule ambao aliokuwa nao siku walipothibitisha ubingwa
wao kwa kuwafunga Aston Villa alipokimbia na kwenda kumdandia mabegani
Van Persie. Huyu hakuwa mchezaji ambaye hakuwa na furaha na mwenye
kutaka kuhama, kwa hakika usingeona kama alikuwa na tatizo lolote.
Lakini huwezi kuwajaji wacheza soka kwa ushangiliaji wao uwanjani bali
ni uchezaji wao na ukweli ni kwamba katika miezi kadhaa iliyopita
kiwango cha Wayne Rooney kimeonyesha kwamba mchezaji huyo hana furaha na
maisha yake ndani ya Man United.
Wakati
Rooney
alipoibuka kwenye ulimwengu wa soka alionekana kuwa na kila kitu cha
kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani. Kwenye Euro 2004
alionekana kuwa na kasi, mwenye njaa ya mafanikio na adui mkubwa wa
nyavu za wapinzani. Uhamisho wa kwenda United ulionekana sahihi kabisa -
sehemu nzuri zaidi ya kukuza kipaji chake, lakini ikiwa karibia muongo
mmoja umepita unaona kwamba Rooney hajafikia kule alipotakiwa kuwa.
Kipaji ambacho kilitoa ahadi kubwa kimekosa msimamo imara.
Je Ferguson ameharibu kipaji?
Unaweza
kumlaumu Alex Ferguson kwa kufeli kwa Rooney kuwa mchezaji wa daraja la
juu kabisa duniani. Cristiano Ronaldo alichaguliwa kuwa mtoto wa
kipekee ndani ya United wakati wawili hao wakiwa chipukizi na Rooney
akawa mlishaji wa Ron kuliko kuwa mchezaji ambaye timu inamzunguka. Ndio
Rooney alikuwa bora, lakini bado Ronaldo alipewa uhuru wa kuwa mchezaji
muhimu wa timu na kujijenga kuwa mchezaji bora kabisa. Rooney akawa
Robin kwa Batman.
Je Ferguson angeweza kujenga timu kwa kumzunguka Rooney na kumsaidia kumjenga kuwa bora kabisa kama alivyotegemea baada ya Euro 2004? Inawezekana kabisa. Lakini Ferguson ni mtu ambaye anaangalia zaidi timu kuliko mchezaji binafsi na imani yake ilimtuma kwamba mafanikio ya timu yangekuja kwa kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji muhimu wa timu. Ni vigumu kubisha ukiangalia namna United walivyopata mafanikio Ronaldo alipokuwepo kama mchezaji anayecheza akiwa huru kwa timu kumzunguka yeye.

Sina
mashaka kabisa kwamba kiwango cha Rooney kiliathiriwa na kucheza kwenye
kivuli cha Ronaldo kwa muda mrefu na akakosa kuwemo katika ile miaka ya
kujiendeleza ambayo ni wachezaji wachache wanapata. Hivyo si sawa
kujaribu kwa sasa kumfananisha na wachezaji aina ya Messi na Cristiano.
Pia Rooney amekuwa akitumika kama 'kiraka' na hilo nalo likamdumaza
chini ya Ferguson.
Sio
wachezaji wengi ambao wanaweza kuwa na ubora wa Rooney - kuweza kucheza
popote pale mwalimu wao anapowataka kufanya hivyo, lakini hilo bado
halikuweza kumfanya kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani.
Kuomba kwako uhamisho
Mwaka
2010 wakati alipoongea hadharani kuhusu timu kukosa hamu ya mafanikio
kwa kutosajili wachezaji wa daraja la juu, aliiweka United kwenye hali
ya utata. Mwaka mmoja baada ya kuwapoteza Tevez na Ronaldo na kuwaleta
wabadala Owen na Valencia ilikuwa wazi kabisa United walishuka kiubora.
Ni kweli alichosema Rooney kuhusu timu yake lakini pia jambo hilo
lilikuwa kinyume kabisa na utamaduni wa United.
Unaweza
ukafikiria namna maoni yale ya Rooney yalivyomkasirisha Ferguson na
kibaya zaidi hakuwa na namna zaidi ya kufanya liwezekanlo na kumbakisha
mchezaji wake tegemeo kuliko kumpoteza kwa Man City - ingekuwa ni tukio
baya sana kwa United na mashabiki wake. Rooney akabakia United, na
akishinda vita yake dhidi Fergie aliyejifanya mdogo na kumuomba Wayne
abaki na tofauti na sera yake ya kuwafukuza wachezaji mastaa waliojiona
wakubwa kuliko timu kama akina Beckham, Keane na Stam. Tangu wakati huo
Rooney amekuwa sehemu ya timu japokuwa sio tegemeo kama ilivyokuwa huku
nyuma.
Kwa matatizo yote ambayo yameonekana kuwepo baina ya Fergie United wameweza kubeba kombe lao msimu huu. Kwa kifupi msimu huu imeonekana wazi United hamhitaji Rooney kuweza kucheza vizuri. Usajili wa Robin van Persie na Shinji Kagawa ulileta maswali ya haraka haraka. "Ni wapi Rooney atacheza?" na ingawa Ferguson amefanya kazi nzuri katika kubadilisha kikosi chake ni wazi kwamba Van Perise ndio kiongozi wa mashambulizi ya timu na Kagawa na Welbeck wapo tayari kucheza kama wasaidizi wake.

Mechi
dhidi ya Madrid zilionyesha wazi; Ferguson aliamua kumtumia Kagawa
kwenye mechi ya kwanza na Welbeck katika mechi ya pili, Rooney
alionekana kuwa angefaa zaidi kucheza kwenye jukumu la kuilinda timu
katika mchezo wa pili. Fundisho lilonekana dhahiri, ikiwa utamkera
Ferguson usidhani atasahau. Msimu wa 2010-11 Ferguson alimhitaji Rooney,
lakini David Moyes ndani ya mwaka 2013 hamhitaji.
Rooney hahitajiki tena
Ferguson
amemuachia Moyes timu nzuri sana yenye mchanganyiko mzuri wa wachezaji
wenye uzoefu na wanaochipukia kuwa wanasoka wenye vipaji vya hali ya
juu.
Kagawa atakuwa bora zaidi msimu ujao na kama akifikia ule uwezo aliokuwa
na Dortmund basi mashabiki wa United wategemee makubwa zaidi.
Ndio
Moyes ataweza kupata changamoto za kuondokana na uzoefu ndani ya timu
katika miaka inayofuatia; Scholes sasa ameondoka, Giggs, Ferdinand, Evra
na hata Vidic wanaweza wakafuata nyayo za Paul Scholes misimu ijayo
lakini bado kuna wachezaji chipukizi ndani ya Old Trafford ambao
wanaonekana kuwa hatma nzuri ndani ya timu.
Swali
kwa Moyes, je Moyes na United wanamhitaji Rooney? Ferguson amesema
kwamba Rooney mwenye uwezo wa 100% angecheza kila dakika lakini bado
siwezi kuacha kufikiria kwamba ooney hatoweza kufia uwezo wake kwa 100%
akiwa ndani ya United na Ferguson anajua hili. Uhusiano wake na klabu
kwa ujumla wakiwemo mashabiki umefikia pabaya. Maombi mawili ya kutaka
kuondoka ndani ya miaka mitatu inaonyesha hali hali ilivyo.
Angeweza kuendelea kukaa na kuwa gwiji wa klabu ilivyo kwa akina Scholes au Giggs, au pia angeweza kuvunja rekodi hata ya Bobby Charlton ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu na kujitengenezea ufalme ndani ya klabu kubwa kabisa duniani. Lakini uweledi mdogo wa Rooney ambao hauvumiliki ndani ya klabu ya aina ya United utamuondoa ndani ya klabu hiyo. Ameshapewa nafasi nyingi za kuwa mchezaji mwenye uelwedi ambaye United wanahitaji lakini ameshindwa. Hali ilivyo sasa kidogo inafanana na ilivyokuwa miaka ya mwisho ya David Beckham ndani ya Old Trafford.

United
ni kubwa kuliko mchezaji yoyote na Ferguson ameonyesha hilo miaka yote
akiwatimua bila huruma wachezaji kama Ince, Keane, Stam, Beckham na Van
Nistelrooy. United
waliendelea kupata mafanikio wakati wachezaji wakiwa hawapo na hakuna
mashaka kwamba United wataendelea kufanya vizuri bila Rooney.
Ni bora zaidi kama ataondoka Old Trafford wakati huu. Moyes atataka kuja kwenye klabu bila kuwepo kwa msongamano wa habari na tetesi zinamhusu mchezaji mmoja kuliko timu yake kwa ujumla. Moyes anahitaji kumwambia Rooney hatoweza kumpa Rooney nafasi anayoitaka ndani ya timu. Kiukweli mfumo wa Van Persie/Kagawa unatoa ishara nzuri zaidi kwa mafanikio ya timu huku Welbeck na Hernandez wakitafuata muda zaidi wa kucheza, Rooney kubaki kutafanya mambo yazidi kuwa magumu kwa Moyes.

Ni
muda wa kukiri kwamba muda wa Rooney ndani ya United umefikia mwisho.
Tena inawezekana amekaa kwa muda mrefu zaidi ilivyotakiwa. Lakini kabla
ya msimu huu United wamekuwa wakimhitaji zaidi Rooney lakini sasa
umuhimu huo umepungua. Hii inanikumbusha sakata la Ronaldinho na
Barcelona mwaka 2008, alikuwa na misimu miwili ya nyuma ambayo alianza
kupoteza fomu yake na ubora na Guardiola alijua kwamba ili kuendelea
mbele ingebidi mbrazili huyo aondoke. Ni vigumu kuacha kuona ufanano wa
suala hili la Rooney na Ronaldinho.
Wapi
ataenda? United hawatomuuza kwa timu ya kiingereza, Man United sio
Arsenal. Na kuwa mkweli kabisa ada ya uhamisho wa Rooney na mshahara
wake unaweza ukaziondoa timu nyingi kwenye mbio za kumsaini ndio maana
sitoshangazwa kumuona akijiunga aidha Madrid au PSG msimu ujao.
Nilisemaga
msimu uliopita Rooney anahitaji kuondoka United kwa maendeleo yake
binafsi kama mchezaji kwa kuwa mmoja ya wachezaji watatu wa kiwango cha
juu duniani. Ingeweza kuwa uamuzi mzuri ambao angeweza kuufanya, pia
uamuzi huo ungemsaidia yeye kukua kama mchezaji na kuisadia timu yake ya
taifa ya England.
United
watatengeneza fedha nzuri kwa biashara ya Rooney na kuondokana na mzigo
wa kulipa zaidi ya £200,000 ya mshahara. Ni jambo zuri kwa pande zote.
Wote wamesaidiana na kufanikiwa katika maisha yao ya pamoja lakini bado
ilivyo kwa mahusiano mengine inabidi ujue wakati wa kuachana.