KLABU za Arsenal na Chelsea zinaweza
zikamaliza Ligi Kuu ya England zikiwa zinalingana kwa kila kitu, pointi
na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa hivyo kulazimika kucheza
mechi maalum baina yao kutafuta timu ya kushika nafasi ya tatu.
Ushindi wa 4-1 wa Arsenal 4-1 dhidi ya
Wigan unamaanisha The Gunners wamefikisha pointi 70 na wastani wa mabao
ya kufunga na kufungwa 34, huku ikiwa imefunga mabao 71 msimu huu.

Mvunja rekodi: Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard ameisaidia timu yake kupaa nafasi ya tatu
Hii inamaanisha ikiwa Chelsea itatoka
sare ya bila mabao na Everton Uwanja wa Stamford Bridge katika mechi ya
mwisho na kikosi cha Arsene Wenger kikaifunga Newcastle kwa wastani wa
bao moja, iwe 2-1, 3-2, 4-3, timu hizo zitalingana kwa kitu.
Kwa kuwa nafasi ya tatu inaifanya timu
ifuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa badala
ya kuanzia kwenye kuwania kufuzu, inamaanisha kushika nafasi ya tatu ni
hatua nzuri.
BIN ZUBEIRY kupitia Sportsmail inatambua kwamba Ligi Kuu England imekwishaanza kuandaa mechi hiyo maalum iwapo itatokea.
Uwezekano wa kumaliza msimu kwa mechi
maalum ulipangwa zamani, rejea msimu wa 1995-96 wakati Manchester United
na Newcastle United zilipokuwa zinagombea ubingwa.
Licha ya mchuano mkali wa jino kwa jino, mwisho wa siku United ilishinda mbio za ubingwa bila mechi maalum.
Licha ya mchuano mkali wa jino kwa jino, mwisho wa siku United ilishinda mbio za ubingwa bila mechi maalum.
Inafahamika kama kutakuwa na mchezo huo
maalum, basi utafanyika mara moja tu msimu utakapomalizika na kwa
vyovyote utachezwa London.
