come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BATAROKOTA AENDELEA KUSOTA JELA

Mwanamuziki wa nyimbo zenye lafudhi ya kabila la Kisukuma Paskal Beatus ama Batarokota (Pichani) bado anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ulaghai, Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia zinasema kuwa Batarokota anadaiwa kumdhulumu ndugu yake kiasi cha shilingi Mil 2.


Alikamtwa na polisi ijumaa iliyopita na kufikishwa mahakamani ambapo alisomewa shitaka, Batarokota alipelekwa gereza la Keko ambapo bado anasubiri hukumu ingawa dhamana iko wazi ila amekosa wadhamini wawii.

Kabumbu Spoti ilizungumza na mke wa wa msanii huyo ambaye pia ni mwandishi wa riwaya na mashairi ambaye alisema kuwa yeye hafahamu chochote kuhusu deni hilo na anashangaa kuona mumewe anafikishwa polisi