MABINGWA wa soka nchini pamoja na ukanda wa Afrika mashariki na kati Yanga wametamba kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa kufunga dimba na mtani wake wa jadi Simba SC utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumamosi.
Akizungumza na Kabumbu Spoti, Msema ji wa klabu hiyo Baraka Kizuguto amesema kuwa Yanga ina kila sababu ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo, Kizuguto amedai kuwa kikosi cha Yanga kimeimarika tofauti na Simba.
'Yanga imekaa pamoja kwa muda mrefu hivyo wachezaji wamezoeana, Pia uzoefu katika mashindano mbalimbali ni sehemu inayochangia kupata ushindi, Msemaji huyo wa Yanga pia alisisitiza na kudai mashabiki wa Yanga wasiwe na hofu yoyote na jumamosi watapata ushindi, Amedai kuwa hata Simba wameanza kupatwa na mchecheto juu ya mchezo huo, Yanga kwa sasa iko Zanzibar ikijiandaa na mchezo huo
