![]() |
|
|
|
Sofapaka walijiinua kutoka kucharazwa mabao 3-0 na AFC
Leopards wiki jana kulazimisha sare tasa na mabingwa wa Ligi Kuu Kenya,
Tusker FC katika mechi yao iliyochezwa Jana katika uwanja wa Nyayo,
Nairobi.
Kocha David Ouma alifanya mabadiliko katika timu yake na kumchezesha Yusuf Juma aliyesajiliwa majuzi mahala pake Collins Kisuya katika safu yao ya ulinzi.
Tusker walitawala kipindi cha kwanza kwa muda mrefu huku mshambulizi wao nyota, Jesse Were, akikosa fursa wazi ya kuwapatia uongozi wakati alipoelekeza mkwaju wake nje.
Mlinda ngome wa Sofapaka, Thomas Wanyama, alipata bahati kubwa kubakia uwanjani pale alipomwangusha Were ambaye alikuwa amepata njia wazi ya lango lakini refa Raphael Nduati alitoa kadi ya njano.
Kiungo wa asili ya Zimbabwe, Obadiah Tarumbwa ndiye aliyenoga upande wa Sofapaka na mashumbulizi kadhaa lakini kipa wa Tusker, Boniface Oluoch alikuwa chonjo.