come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PATA SABABU ZILIZOMUONDOA STEPHANO MWASYIKA YANGA

Nguzo nyingine inayoangushwa Jangwani, Siri ya kutemwa kwake yabainika

WIKI iliyopita niliwapa nafasi ya kuchambua mambo machache yanayomuhusu beki namba mbili Shadrack Nsajigwa 'Fusso', Tena mliona umhimu wake katika timu ya taifa, Taifa Stars, Kukosekana kwake kumechangia kufanya vibaya kwa timu ya taifa.


Watanzania sasa wamelitambua tatizo lililopelekea kufanya vibaya kwa timu yao, Katika mechi mbili zilizofanyika mfululizo ikianza ile ya mjini Marakech dhidi ya Morocco ambapo Stars ililala mabao 2-1.

Ikiwa imecheza kandanda zuri la kuvutia huku asilimia mia moja Stars ikiwafunika Morocco lakini tulishangaa tukipoteza mechi hiyo, Na tukaanza kupeleka lawama kwa mwamuzi wa mchezo hui kwa madai ya kuwapendelea wenyeji.

Na katika mchezo mwingine wa marudiano uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mambo ni yale yale kucheza tumecheza sisi kufungwa tumefungwa sisi, Kila mmoja wetu alishangazwa na matokeo hayo.

Ingawa lawama nyingine zilzianza kupelekwa kwa mwamuzi kwa madai ya kuwapendelea Ivory Coast. Lakini nimeanza kuwasifu Watanzania kwa kuchunguza kwa makini na kugundua tatizo lililopo.

Ndipo kocha wa timu ya taifa Kim Poulsen alipoamua kufanya mabadiliko ya kumuita beki wa upande wa kushoto toka Yanga David Luhende ili kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo, Matatizo makubwa yanayoigharimu Stars ni kukosekana kwa mabeki wa pembeni ili kusaidiana na mabeki wa kati na kuunda ukuta mgumu usiopitika.

Lakini muda si mfupi nadhani katika miaka ya 2006/11 ukuta wa timu ya taifa uliweza kuimarika vilivyo, Ukuta huo ulikuwa ukiongozwa na nyota kadhaa, Ikiwa chini ya Mbrazil Marcio Maximo, Stars ilikuwa moto wa kuotea ,mbali na makosa madogomadogo hayakuweza kuonekana.

Kama tumefungwa na timu pinzani basi ushindi huo ni wa kihalali na wala hakuna mkono wa mtu, Makosa ya kizembe hayakuweza kutokea kwani kila mmoja alikuwa makini katika nafasi yake uwanjani.

nNi jambo la kushangaza sana kuona makosa yakitokea kirahisi, Na bado Stars ilikuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali hasa kutokana na kutomimarika iapasavyo kila idara, Kwa sasa tatizo hilo halipo tena ila ukuta wake unalegalega.

Maximo alijilingia kikosi bora kabisa ambacho kiliweza kuzitingisha timu ngumu kama Ghana, Cameroon, New Zealand, Burkina Fasso na nyinginezo kadhaa ambazo zilikuja kucheza na Stars.

Watanzania walikuwa wakipata raha kutokana na matokeo mazuri iliyokuwa ikiyapata timu yao kiasi kwamba ilialikwa na bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya spika mstaafu Samuel Sitta mjini Dodoma.

Stars ilipata nafasi hiyo ya kualikwa na waheshimiwa wabunge kutokana na matokeo mazuri iliyokuwa ikiyapata, Kuanzia miaka hiyo hadi sasa bado Stars inacheza soka la jukwaani na imeshindwa kuwafurahisha waheshimiwa wabunge hadi kualikwa kwa mara nyingine.

Spika wa sasa Anne Makinda naye anataka kuwaona wachezaji wa timu ya taifa ili aweze kujivunia, Lakini vijana wanamuangusha, Hata Kim Poulsen naye anapenda kukutana na wabunge ili kudhihirisha kuwa yeye ni kocha bora ila ndoto hazijatimia.

Ukuta wa Stars ulikuwa ukiongozwa na Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan au Victor Costa Nampoka 'Nyumba', mabeki wa pembeni waliongozwa na Shadrack Nsajigwa aliyekuwa akicheza kulia na Stephano Mwasyika akicheza kushoto.

Safu ya ulinzi ya timu ya taifa ilionekana iko thabiti, Klikuwa hakuna uchochoro hata kidogo, Kipindi hicho Mwasyika alikuwa akikipiga na timu ya Moro Uited akiwa ametokea Tanzania Prisons ya Mbeya.

Yanga iliamua kumsajili baada ya kumuona aking'ara kwenye timu ya taifa, Akiwa katika kikosi cha Yanga, Mwasyika alionyesha ushirikiano na wenzake hatimaye kuiwezesha Yanga kutwaa mara mbili mfululizo ubingwa wa vilabu Afrika mashariki na kati maaerufu kama kombe la Kagame.

Klabu ya Yanga inataka kufanya kosa moja kubwa tena sana kwa kutaka kumuacha katika usajili wake msimu ujao beki wa kupanda na kushuka Stephano Mwasyika, Hilo litakuiwa kosa kubwa endapo Mwasyiks atachukuliwa na timu pinzani.

Mwasyika ni mmoja kati a mabeki bora kabisa hapa nchini ambapo kiwango chake bado kipo imara na wala hakijashuka tofauti na inavyoenezwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitangaza kushuka kwa kiwango cha soka la Mwasyika.

Mwasyika hakuwa chaguo la kwanza la kocha Ernie Brandts hivyo umuhimu wa kuendelea kumtumia haupo tena na kilichobaki na kumnyooshea njia ya kupita, Mwasyika ni nguzo muhimu inayoangushwa Jangwani.

Kutokuwepo kwake uwanjani katika kikosi cha Yanga kumesababisha udhaifu mkubwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambapo umuhimu wa mchezaji unaanzia kwenye klabu yake ndipo huteuliwa Stars.

KIPI KINAMUONDOA YANGA!

Kuna taharifa kuwa Mwasyika anaondoka Yanga kwa sababu ya kutoelewana na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kongwe barani Afrika, Hakuna maelewanoi mazuri baina yake na kiongozi mmoja wa Yanga ambaye anasikilizwa sana.

Na sababu kubwa iliyokuja kubainika ni kutokana na uhamisho wake kutoka Moro United kuja Yanga, Kiongozi huyo inadaiwa aliwahi kuwa kiongozi wa Moro United hivyo alimtaka Mwasyika ampe kiasi cha pesa alicholipwa na Yanga na baada ya Mwasyika kukataa kumpa bifu baina yao likaanzia hapo.

Na sasa kiongozi huyo anaelewana sana na uongozi uliopo madarakani na ndio maana matatizo dhidi yake yameanza kujitokeza pamoja na kuwekwa benchi kwa idhini ya kigogo huyo