come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Taasisi ya vijana inavyojikwamua kimaisha

Taasisi ya vijana ya Young Survivors Group iliyopo Tabata Mtambani jijini Dar es Salaam, yenye Kuwajengea uwezo na kuwawezesha vijana kuchukua hatua itakayowasaidia kunufaika na fursa zinazopatikana.


Akizungumza hayo, Mwenyekiti wa Young Survivors Group Steven Kalanje, (Pichani) amesema kuwa Vijana watejengewa uwezo wa kuziona na kuzitumia fursa mbalimbali kwa kupewa elimu ya ujasiliamali, aidha Kalanje, amefafanua kuwa vijana watafundishwa namna ya kufanya utafiti wa soko ili kuweza kutambua mawazo fasaha ya biashara.

Aliongeza kuwa elimu ya kutengeneza mpango wa biashara itatolewa kwa vijana itakayowajengea uwezo wa kutambua faida na hasara ya biashara kabla ya kuianza. Pia vijana wataweza kukutanishwa na Tasisi za fedha ili waweze kupata fursa za kupata mikopo.

Kalanje aliyasema hayo wakati wa mkutano maalum na taasisi RESTLESS DEVELOPMENT  ambayo inajishughulika na kuwajengea uwezo vijana, uliofanyika 18/06/2013 Tabata.

Restless Development walifanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ya vijana iliyowezeshwa kupitia Young Survivors Group, pia wasanii wa nyimbo na maigizo waliweza kutumbuiza.

Naye mmoja kati ya vijana waliowezeshwa na elimu ya ujasiliamali Saleh Mustapha amesema kuwa mpaka sasa ameweza kupiga hatua katika ufugaji hivyo unaweza kumkomboa kimaisha kama kijana, 'Kwa sasa sikai tena kijiweni, nimewekeza katika ufugaji napiga hatua', alisema Mustapha alipotembelea na taasisi hiyo ya kimataifa ya Restless Delevopment