Mabingwa watetezi Yanga, Simba na Super
Falcon ya Zanzibar zinataraji kushiriki katika michuano hiyo ya mwezi
ujao ambayo imepangwa kucheza katika vituo viwili vya Alfashery, mji wa
Darfur kaskazini, na Kadugli.
Akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika
kuchangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
jana Bungeni hapa, Bernard Membe alisema:
Hali ya usalama ni ya wasiwasi (Darfur)
kwa sababu watu wanaokwenda huko wanapokewa na vikosi vya magari
yasiyoingia risasi na huvishwa nguo ambazo hazipenyezi risasi.
“Wageni wote wanaokwenda Darfur huwa
wanapokelewa na magari ambayo ni bullet proof (yenye kuzuia risasi) na
wanapewa t-shirt zenye bullet proof,” alisema na kuongeza:
"Nimeshangaa mipango hii ya kupeleka
wanamichezo huko bila maandalizi makubwa na si kwa upande wetu (bali)
wale walioandaa michezo hii Darfur.”
Shirikisho la soka la Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA) ndilo lililopanga vituo viwili hivyo vya nchini Sudan kwa
ajili ya michuano hiyo ya kila mwaka.
Katika Kombe la Kagame, Yanga imepangwa katika Kundi C pamoja na timu za Express (Uganda), Ports (Djibout) na Vital’O (Burundi).
Simba ipo kwenye kundi A pamoja na timu za El-Merrekh (Sudan), APR (Rwanda) na Elman (Somalia).
Kundi B lina timu za Al-Hillal (Sudan), Tusker FC (Kenya), Al Nasri (Sudan Kusini), Falcon (Zanzibar) na Al Ahly Shandy (Sudan).
Mechi za Kundi A na C ndizo zitachezwa Alfashery.
Membe alisema anashangaa busara
iliyotumiwa na CECAFA kuchagua jimbo la Darfur kuwa sehemu ya kufanyia
mashindano hayo kwa sababu "usalama wa vijana utakuwa katika mashaka."
"Kwanini wamechagua kuwa sehemu mojawapo ya kuchezea mechi?”